8. Amekuja Mwokozi
K: /:Amekuja
W: mwokozi.:/
K: /: Ufalme wa juu karibu.
W: Amekuja mwokozi. :/
K: /:Geukeni
W: mioyo. :/
K: /:Watatupwa wenye kiburi.
W: Geukeni mioyo. :/
K: /:Shoka lipo
W: shinani, :/
K: /: Mti usiozaa wakatwa.
W: shoka lipo shinani.:/
K: /:Ana ungo
W: mkononi,:/
K: /:kupepeta ngano yake.
W: Ana ungo mkononi.:/
K: /:Yatachomwa
W: Makapi,:/
K: /:Ngano yawekwa chanjani.
W: Yatachomwa makapi:/
K: /:Nabatiza
W: Kwa maji,:/
K: /:Yeye hubatizwa kwa Roho.
W: Nabatiza kwa maji.:/
K: /:Mbele yake
W: Sifai,:/
K: /:Kumfungulia viatu.
W: Mbele yake sifai.:/
K: /:Elekea
W: Mbinguni,
K: /:Kristo katufanyia njia.
W: Ya kwendea mbinguni.:/
Comments
Post a Comment