9. Faraja, Tumaini Langu



Faraja tumaini langu

Usiniache gizani,

Moyo ni wazi kukungoja,

Ee Yesu uniingie,

Furaha ya mbingu na nchi,

Mwana Adamu na Mungu;

Ee nuru kutoka mbinguni,

Angaza moyo wangu huu.


Mototo mpendwa,

Nakuomba,

Chagua moyo wangu huu,

Ufanye  kuwa horilako

Ukalazwe humo wewe.

Ili nipate mwisho mwema

Wa shida yangu na vita.

Zaliwa ndani yangu Yesu,

Na ndani yangu ukuwe.


Mwokozi wangu utulize

Tumaini hili kubwa.

Ukija nitakupokea

Kwa roho nyenyekevu, hii.

Uweza wangu wote pia

Wakungojea kwa uchu.

Nataka kukutumikia:

Njoo, Yesu usikawie .

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu