83. Yesu, Kuteswa Kwako
Yesu, kuteswa kwako nitakufikiri
Nipe kwa shauri hili
Roho na mbaraka.
Moyo wangu uone hali yako Yesu
Jinsi ulivyoteswa
Kwa ajili yetu.
Moyo wangu uone
Taabu yako kubwa,
Maumivu, mapigo,
Na kuwambwa mtin,
Taji lako la miiba
Tena misumari,
Iliyokuumiza,
Hata kufa kwako.
Nikitazama yote
Yaliyokutesa,
Nifikiri sababu
Na maana yake.
Sababu ndio mimi
Na makosa yangu;
Umepata mateso,
Nipate huruma.
Yesu unifundishe
Nijui kwa moyo;
Nisikuzidishie
Shida na uchungu.
Nisiweze kupenda
Yaliyokutesa:
Nataka kuyaacha
Na kukufuata.
Comments
Post a Comment