76. Mwana Kondoo Ayalipa
Mwana Kondoo ayalipa
Madeni ya dunia.
Ayachukua makosa
Ya wakosaji wote.
Aenda na kuugua,
Anakubali kuchinjwa,
Furaha aziacha.
Wanamhukumu wampiga,
Wanamtukana wamtesa,
Asema: nakubali.
Mwana Kondoo ni Mwokozi
Ni Mponya wa mioyo;
Aliyetumwa na Mungu
Awakomboe watu.
Mwanangu, nenda okoa
Watoto niliotupa.
Sababu ya makosa.
Dhambi zao ni nyingi mno;
Watolee ukombozi
Damu na mwili wako.
“Tayari mimi, Babangu,
Nitwishe nichukue,
Maneno uyasemayo
Nitafuata yote”
Pendo hili kubwa sana,
Lamsjika Baba wa mbingu
Amtoe mwana wake.
Pendo hili lina nguvu,
Linamlaza kaburini
Aletaye uzima.
Sitasahau pendo hili
Bwanangu siku zote,
Nitakushika daima,
Kama unishikavyo.
Mwanga war oho ni wewe;
Roho inapozimia
Niwie moyo wangu.
Na tuagane, Bwanangu,
Na halafu mbingini.
Comments
Post a Comment