5. Nikulakije Vema


Nikulakje vema

Bwan wangu Yesu

Wote wanakungoja

Wapewe uzima.

Nuru yako ing’aze

Hata moyo wangu.

Nijue mabo mema,

Yakupendezayo.


Wamekutandikia

Mauwa na nguo.

Name nakuimbia

Nyimbo za furaha.

Moyo ukupendeze

Kwa sifa na nyimbo,

Ukakutumikie

Sikuzangu zote


Umetoka Mbinguni

Ukawa masikini

Ukaacha fura

Utupe uzima.

Natulipo nyang’anywa

Ufalme na raha,

Ukaja mponya wetu

Kuturudishia.


Nalifungwa na mwovu,

Ukanifungua.

Nikawa nimetwezwa,

Ukanitukuza,

Ukanifanya mkubwa,

Ukanipa mali,

Zisizo malizika,

Kwa kutu na wezi.


Umenijia mimi,

Sababu ya nini?

Sababu ya kupenda

Uwaponye wote

Waonao huzuni

Kwa makoso yao

Wakijuta kwa kweli,

Utawapokea.


Ushike neon hili,

Umati wa Yesu,

Ukiwa na huzuni

Na shida popote.

Usiogope kitu;

Wokovu tayari.

Anaye tufariji

Yukaribu sasa.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu