84. Nimshangilie Bwana Wangu
Nimshangilie Bwana wangu
Na kumwimbia Mkombozi
Katukomboa msalabani,
Nisifu pendo lake kuu
Haya mwimbieni Yesu,
Amekubali mateso,
Katukomboa msalaabani,
Tusifu pendo lake kuu!
Tumsifu yeye
Mponya wetu
Katika ulimwemgu huu,
Katupatanisha na baba,
Tulio wakosaji tu.
Haya mwimbieni …
Katuletea mwanga wake,
Tulikaa katika giza,
Wokovu ukaonekana,
Kamshinda mwovu,
Ni shujaa!
Haya mwimbieni …
Na tumtukuze Bwana wetu,
Tumtumikie kwa bidii,
Na atawale apendavyo,
Na sisi sote tutamtii!
Haya mwimbieni …
Comments
Post a Comment