100. Mungu Tusaidie



Asili ya Wimbo: Haijulikani


Mungu tusaidie,

sisi tunaangamia.

Nchi imeharibiwa na

mwovu wake shetani.

Kweli kweli ndiye

Yesu aliyewambwa mtini

penye mlima wa Golgotha

aokoe wenye dhambi.


Kaonyesha huruma,

wayuda wamsumbua.

Wakampiga makofi,

Pilato aliamua.

Kweli kweli ndiye Yesu


Yesu mwenye upendo

alikubali kuuawa, damu ilimwagika

ili sisi tuokoke.

Kweli kweli ndiye Yesu.


Pale msalabani, Bwana Yesu

aliteswa mzigo wa dhambi zetu

ulimwangukia yeye.

Kweli kweli ndiye Yesu


Sote na tukumbuke,

kifo cha Mwokozi wetu.

Alisema ya kwamba jililieni wenyewe.

Kweli kweli ndiye Yesu


Habari zilisemwa.

Mahali hapa hayupo, ona alipokuwa,

jiwe limeondolewa.

Kweli kweli ndiye Yesu


Ni ajabu kabisa wingu kuja kumpokea,

habari ilisema Yesu atarudi tena.

Kweli kweli ndiye Yesu

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu