51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu



Yesu ndiye kiongozi

Wangu,

Kumfuata yeye ni furaha,

Ajuaye kuongoza vema,

Anilinda, nisione shida,

Analeta raha moyoni.

Bwana yesu

Akiniogoza,

Nitapita pori na misitu,

Nitavuka mito na bahari

Kwa furaha,

Kwani nina njia

Yakufika mjini kwa Mungu.


Nikilala Yesu anilinda,

Anitunza yeye siku zote.

Hata nikifika njia panda,

Nikiona shaka, aonyesha

Njia ya kufika kwake.


Siku zote namfuata yeye,

Sitaona kiu wala njaa;

Anitunza kwa rehema

Nyingi;

Nitaweka mikononi mwake

Moyo wangu, auokoe.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu