98. Mungu Ameona Tulivyo



K: Mungu ameona

W: Tulivyo huku chini,

K: Neno hilo jema

W: Litokalo mbinguni Ya kwamba

Yesu kaja na kutuongoza,

tufike uzimani.


K: Hujui njia

W: Uende upande gani

K: Nuru yake Bwana

W: Huangaza njiani. Ya kwamba Yesu


K: Kweli, unajua,

W: Mtu wa duniani.

K: Atakuongoza

W: Upate kuamini. Ya kwamba yesu.


K: Njooni tufungue

W: Milango ya moyoni

K: Neno lake Bwana

W: Likaingie ndani. Ya kwamba Yesu

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu