42. Ilitoka Nuru Kuu


Ilitoka nuru kuu,

Kuliko nuru zote;

Na huo wimbo wa juu

Wapiti nyimbo zote;

Ndiyo habari tukufu,

Ya Kristo wa utukufu,

Awajia wapole;

Ni Mungu pamoja na sisi

Imanueli.


Mwaka huandama

Mwaka,

Wimbo huo na uimbwe;

Wapenda kukumbuka,

Mzee na wanawe,

Ndiyo habari tukufu,

Ya Kristo wa utukufu,

Awajia wapole;

Ni Mungu pamoja na sisi,

Imanueli.


Twafurahi siku hii

Ijavyo kila mwaka;

Nasi tufanye bidii

Huku tukikumbuka,

Ndiyo habari tukufu,

Ya Kristo wa utukufu,

Awajia wapole;

Ni Mungu pamoja na sisi

Imanueli.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu