190. Onjeni, Onjeni
1. K: Onjeni, onjeni.
W: Onjeni muone kuwa Bwana ni mwema, onjeni.
K:heri. W:Anayemtumaini,
K: Heri
W:Anayemtumaini, ni heri.
2. K: Mcheni, mcheni.
W: Mcheni Bwana, mlio watakatifu, mcheni.
K:Wale
W: Wanaomcha Bwana
K:Wale
W:Wanaomcha Bwana ni heri.
3. K: Na samba, na samba.
W: Na samba hutindikiwa, huona njaa na samba.
K: Bali
W: Wamtafutao Bwana,
K: Hawa
W: Hawahitaji kitu, chochote
4. K: Njooni, njooni,
W: Njooni, enyi wanangu, nisikilize njooni.
K: Nanyi
W: Mtamjua Bwana,
K: Nanyi
W: Mtamjua Bwana, njooni
5. K: Ni nani, ni nani?
W: Ni nani apendezwaye nao uzima, ni nani?
K: Mwenye
W: Kupenda siku nyingi,
K: Mwenye
W: Kupenda siku nyingi za mema.
6. K: zuia, zuia.
W: Zuia ulimi, sema yaliyo kweli, zuia.
K: Hata
W: Htaa midomo bila hila
K: Hata
W: Midomo bila hila, zuia.
7. K: Uache
W: Uache mabaya tenda mapenzi yake, uache
K: Nawe
W: Ufate amani,
K: Nawe
W: Utafute amani, amani.
Comments
Post a Comment