236. Neno Lako Bwana Wetu
1. Neno Lako Bwana Wetu, umande wa mioyo, uinyweshe miche yote katika shamba lako. Ikinyweshwa itakua, baadaye itazaa, matunda mema sana.
2. Neno lako ni upanga linapenya mioyo ni shoka kali, lachanja kiini na mifupa. Twakuomba; neno lako lokomeshe makosa litusafishe sisi.
3. Neno lako Bwana wetu ni nyota yenye nuru. Linafundisha wajinga, wajue njia yako.nuru yako itung’aze isizimike kwetu; ila ituangaze.
4. Uwape watu wote njaa ya kusikia neno. Uwape kiu ya roho walikubali hilo. Neno lako lashibisha wanaolitumia, kuwa chakula chao.
5. Neno lako litangazwe katika pande zote, utume mitume wengi walihubiri pote uwaamshe walalao walikubali wote neno lenye uzima.
Comments
Post a Comment