235. Ukae Kwetu Bwana
1. Ukae kwetu Bwana na rehema yako, shetani asiweze kutudhuru tena.
2. Ukae kwetu Yesu na neno la kweli, tupate ukombozi tukilifuata.
3. Ukae kwetu nuru na mwanga wa mbingu, utuongoze njia iendayo kwako.
4. Ukae kwetu Bwana mwenye enzi yote, utupe nguvu nyingi tukutumikie.
5. Ukae kwetu mponya na nguvu yako kuu, adui na dunia wasituharibu.
6. Ukae kwetu Mungu na ukweli wako, tusikuache wewe. Utupeleke juu!
Comments
Post a Comment