233. Mungu Yupo Hapa
1. Mungu yupo hapa, na tumsujudie, tumche tukamtumikie. Yu pamoja nasi, nyamazeni wote tumlalamikie mponya. Wanaolitaja jina lake, njooni, tumpeni sadaka.
2. Mungu yupo hapa, anayesifiwa na malaika kila siku. Wote wanaimba: Mungu Mtakatifu, aheshimiwe popote. Ee Mungu sikia tukikuimbia na sisi wadogo.
3. Twataka kuacha mambo ya dunia na uzuri wake wote. Mioyo na mapenzi hata nia zetu tunakutolea Bwana. Wewe tu, u Mungu, anayestahili sifa za viumbe.
4. Mwokozi ingia, mioyo yetu yote, iwe nyumba yako wewe, ndiwe Bwana wetu, utusaidie tukupende siku zote tukiwa wako tu tukae na wewe tukusujudie!
Comments
Post a Comment