232. Haleluya, Nakusifu



1. Haleluya, nakusifu Mungu uliyenipa leo tena siku yako, ishindayo nyingine, inanifurahisha moyo wangu kabisa.


2. Ninaacha masumbuko; leo siku Bwana. Ninamtumikia Mungu, kwa nguvu zangu zote. Leo vyote havifai ila kazi ya Mungu.


3. Ubariki neno lako linapohubiriwa, liingie mioyoni, watu wategemee. Nyimbo hata maombi yakufikie Mungu.


4. Unisaidie Bwana nimalize siku hii kama nilivyoianza nikikutumikia. Mwisho nione kwkao sikukuu ya milele.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu