231. Mungu Kanilinda Mimi
1. Mungu kanilinda mimi kwa wema mpaka leo. Alinda mwili na roho usiku hata mchana. Aniongoza kila saa, apenda kunibariki na kunisaidia.
2. Ninakushukuru Mungu sababu ya rehema, uliyonifanyizia Bwanangu siku zote. Ninakumbuka daima mambo unitendeayo, ukanisaidia.
3. Uzidi kunibariki, kwa wema wako Bwana. Nisaidie kila saa na mahali popote. Nimshike Yesu Mwokozi, hata na siku ya kufa nipate mwisho mwema.
Comments
Post a Comment