227. Kaa Nami ni Usiku Tena



1. Kaa nami, ni usiku tena; usiniache gizani, Bwana: msaada wako haukomi; nili peke yangu, kaa name.


2. Siku zetu hazikawi kwisha, sioni la kunifurahisha; hakuna ambacho hakikomi, usiye na mwisho, kaa name.


3. Nina haja nawe kila saa; sina mwingine wa kunifaa; mimi nitaongozwa na nani ila wewe? Bwana, kaa name.


4. Sichi neno uwapo karibu nipatalo lote, si taabu; kifo na kaburi haviumi; nitashinda kwako, kaa name.


5. Nilalapo nikuone wewe, gizani mwote nimulikiwe; nuru za mbinguni hazikomi, siku zangu zote kaa name.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu