226. Nimechoka Kabisa
1. Nimechoka Kabisa macho yangu mazito; macho yako Babangu, yanilinde usiku.
2. Niliyokukosea, Mungu niondolee! Damu ya Yesu Kristo huning’aza kabisa.
3. Ndugu zangu, ee Mungu, uwalinde usiku; wakubwa na wadogo wote walale raha.
4. Wenye shida tuliza, uwafute machozi, uwapokee wote wafao usiku huu.
Comments
Post a Comment