225. Mchunga Wangu Mwema
1. Mchunga wangu mwema, huna usingizi unakesha tu. Baba, nimeona neema yak oleo mchana kutwa huu. Hata na usiku huu utawatuma malaika, wanilinde mimi.
2. Uwalinde tena baba na mamangu, nao ni wako. Utufiche sisi mikononi mwako, tusiogope! Njoo Bwana, tuungane: mimi kwako, nawe kwangu hivyo nitalala.
3. Linda mlango wangu na huzuni zangu niondolee. Unikumbatie ndani ya mabawa yako nilale. Unifiche vizuri: ndivyo mwovu hataweza kunikaribia.
4. Baba, ukitaka kuniita mimi leo usiku, nitaweka roho mikononi mwako uipokee. Nitalala kwa raha, kwani wewe wanilinda leo hata kesho.
5. Sasa nitalala kitandani mwangu kwa furaha tu. Roho na maisha nimeweka kwako, mlinzi ni wewe. Kwa heri unilinde! Kama inaamka kesho, wewe huniachi.
Comments
Post a Comment