224. Kukichwa Watu Wote
1. Kukichwa watu wote na wanyama nyumbani na ndege walala. Ee moyo wangu sasa uanze kufikiri ninavyompendeza Mungu.
2. Jua limeingia, giza limetokea, usiku karibu. Jua linguine sasa lang’aza moyo wangu: ni Yesu Mwokozi wangu.
3. Miguu hata mikono inafurahi sana, kazi imekwisha. Nao moyo wataka kukombolewa hivyo katika nguvu za mwovu.
4. Nafumba macho yangu, nalala usingizi, sijui lolote. Wewe uangalie roho na mwili wangu, uliye mlinzi wetu mkuu.
5. Yesu furaha yangu, unifunike sasa, unikumbatie. Uagize malaika wanikingie shida, shetani akinitaka.
6. Hata wapenzi wangu nawaombea wote wasione shida. Mungu atawalinda kwa jeshi la malaika walale wote kwa raha.
Comments
Post a Comment