223. Jioni Moyo Wangu Wakutafuta



1. Jioni Moyo Wangu Wakutafuta Bwana, na kukushukuru. Unikazie macho yenye Baraka nyingi, ung’aze mwili na roho.


2. Natumaini tena rehema yako Baba hata usiku huu. Fukuza majaribu na hila ya Shetani, ukiwa karibu yangu.


3. Unanipenda sana, wakaa pamoja name, wanikaribisha. Kwa wema wako mwingi, sababu hii nakusifu.


4. Maisha yanapita upesi, ni safari ya kwenda mbinguni. Unifundishe, Bwana, kuelekea kwako; pazuri ni mbinguni tu.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu