222. Bwana, Imepita Tena



1. Bwana, imepita tena siku moja ya neema. Nifundishe nifikiri mambo yote ya leo. Unionyeshe sasa niliyokukosea. Nimalize mambo yote kadiri ya mapenzi yako.


2. Kweli utaona mengi yasiyokupendeza. Kwani ni mtu wa makosa, yaliyo mengi sana. Moyo wangu, na kinywa na mikono yakosa kwa kuwaza na kusema na kutenda kila siku.


3. Nakuomba ewe Mungu nihurumie tena. Ondoa maovu yote niliyokutendea. Uyafute makosa kwa rehema yako kuu. Nitaangalia kesho nizishike amri zako.


4. Bwana wewe unakesha, sisi tukisinzia. Macho yako hayachoki, ndiwe Mchungaji mwema, awalindaye kondoo katika giza lote. Utullinde sisi sote, kondoo wako tulalapo.


5. Kukipambazuka tena niondoke kwa bidii nikutumikie vema katika mambo yote; utakaponiita nife leo usiku, ninakuwekea Bwana, roho mikononi mwako.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu