221. Ee Bwana Mungu Mkuu



1. Ee Bwana Mungu mkuu uliye muumbaji, Yesu uliye mwenye fahari, ninajitolea sasa na milele nakupa roho na mwili wangu maisha yangu nakupa wewe, vyote na vyote vilivyo vyangu, ninakutolea kwa furaha.


2. Mionzi ya jua na mwanga wa mwezi vyatoka nuruni mwako Yesu. Na Jeshi ndilo taji zuri kichwani kwako mfalme wa mbingunivyote na vyote ulimwenguni. Asili yao kwako ee Yesu: vyote vyahubiri ukuu wako.


3. Umechaguliwa kuwa kimbilio la watu wenye shida na dhambi. We wasaidia, dhambi waondoa, japo mashaka yakiwa mengi, hatari zote watukingia. Kwa nguvu yako kuu ya kimbingu.


4. Toka duniani twakuelekezea macho yatamani. Mfalme Yesu. Sisi tu gizani, Nawe u nuruni, utuangaze mioyo yetu. Uthibitishe mwenendo wetu, ili mwishoni tusikose, tufike wote mbinguni juu.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu