220. Naamka Mimi Tena
1. Naamka mimi tena kwa nguvu na afya. Na moyo wangu Baba, wakusifu wewe.
2. Baraka na Furaha popote zimejaa, zatoka kwako wewe zimetuingia.
3. Twaimba sifa zako kwa mioyo na vinywa, miti, wanyama wote, wakusifu Bwana.
4. Na sisi twapaliza sauti zetu sasa, maisha yetu yote yawe sifa pia!
Comments
Post a Comment