219. Asubuhi na Mapema



1. Asubuhi na mapema nakukaribia, kukushukuru, ee Bwana, kwa uzima wangu.


2. Uliyenipa usiku kulala ni mzima, nakuomba sasa, Mungu, unilinde mchana.


3. Nilinde majaribuni, kwani sina nguvu, hivi leo maovuni uwe ngao yangu!


4. Katika maneno yangu nisiseme uongo, macho yako Bwana Mungu, yanitunze mimi!


5. Njia yangu nipitayo wewe uwe name, kila niendako leo uwe kiongozi!

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu