217. Ee Yesu Mesiya


1. Ee Yesu Mesiya, Usiku umekwisha. Mwanga wa huruma, wanizunguka tena. Vyote vimeamka, vyakusifu wewe, hata mimi Yesu, ninakutukuza!


2. Ninaamka sasa nazivaa nguo zangu, hata roho yangu, uipambae mwenye, wongofu na pendo na uvumilivu view pambo langu, univike hivyo!


3. Uliye popote ukae hata kwangu, nilinde kwa wema katika njia zangu! Nikusifu wewe kwa mwenendo wangu, kwa neno na tendo siku zangu zote.


4. Nakuomba tena: Uzibariki vema kazi zangu zote ninazofanya leo! Naye Roho wako atawale kwangu, niwe mtoto wako. Hapa na huko juu.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu