215. Tumsifu Bwana Sote
1. Tumsifu Bwana sote tumpendao tumshangilie kwa furaha kubwa na kumtolea sifa na shukrani. Tumsifu Bwana!.
2. Aliyelinda nguvu na uzima aliyetupa Yeye leo tena. Ametuamsha wenye hali njema. Tumsifu Bwana,
3. Tukitumia nguvu za maungo, tukisikia na kusema sawa ndiyo Baraka na huruma yake. Tumsifu Bwana!
4. Mchungaji mwema, atupaye yote, twaomba: Utulinde hata leo, tuone wingi wa rehema yako. Tumsifu Bwana!
5. Tusaidie, tufuate leo kwa nguvu zako njia za kunyooka, tusikuache na rehema yako. Tumsifu Bwana!
6. Utufundishe kusikia Neno na kulishika kwa mwenendo mzuri. Tusaidie tulio wanyonge. Tumsifu Bwana!
7. Utuongoze, tusikose njia tuwe watawa hapa duniani, tukikumbuka siku ya hukumu. Tumsifu Bwana!
8. Siku ya mwisho utakuja Bwana, na kuongoza wateule wako pale malaika wote waimbapo. Tumsifu Bwana!.
Comments
Post a Comment