214. Tokea Nuru ya Mchana


1. Tokea Nuru ya Mchana, uamshe mwili na roho kwa mwanga wako mzuri. Tokea nuru ya roho.niimbe wimbo wa sifa wa kumshukuru Mungu Mungu. Mwimbieni kwa furaha mwenye Enzi alindaye na kuwabariki watu.


2. Ninakushukuru Mungu kwa moyo wote sababu ya neema kubwa. Umenulinda usiku  mwili na roho vizuri kwa jeshi la malaika. Nikaweza kuondoka kitandani kwa furaha mwenye nguvu na uzima.


3. Ninakuomba Babaangu, uyaondoe makosa yangu, hofu na shida kwangu. Niamke hata rohoni, kwa neema yako na rpendo nitakutumikia. Niomgoze nifikiri, mambo yangu mbele yako, nipate Baraka yako.


4. Ee Yesu, uniongoze nishike njia yako tu maisha yangu yote. Ulinde mwili na roho uangalie mwenendo nisianguke leo. Mpenzi wangu, nifundishe, nikumbuke pendo lako, nisishindwe na dunia.


5. Unitawale kwa roho unionyeshe mwenendo kwenda kwako mbinguni. Unibariki popote katika kazi na raha, nipe riziki yangu. Mpaka mwisho niondoke duniani kwa furaha, nikushukuru mbinguni.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu