213. Nakushukuru Mungu


1. Nakushukuru Mungu kwa kinywa na moyo saa hii ya asubuhi hata siku nzima. Nitakuimbia, nitakusifu Baba, alivyonifundisha Mwanao wa pekee.


2. Umenilinda Bwana, usiku kucha huu ukaondoa shida, hatari na msiba. Nakuomba sasa: Uondoe makosa niliyokukosea kwa neno na tendo.


3. Nilinde hata leo kwa neema yako tu, asinishinde mwovu kwa hila yake kuu. Nisione shida ya moto nay a maji, ya homa na ugonjwa, ya kufa kubaya.


4. Mungu atanitunza aliye Mwenyezi, ayabariki yote nitakayotenda. Namwekea Yeye uzima hata kufa, anitendee yale yanayompendeza.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu