212. Bwana Twakuomba Sasa
1. Bwana twakuomba sasa, tutoke sisi hapa, kwani siku yak oleo. Tupe, kufikiri vema Neno lako la uzima, mna la ukombozi wetu sisi tuliopotea tupate kurudi kwako.
2. Yawe mbali kwetu sasa kila mambo masumbufu. Roho na mioyo yetu ikaongee na Mungu. Tupate kutiwa hamu ya raha iliyo kwako, itakayotutokea baada ya maisha haya.
3. Naona kitini pako taji yao washindao; nasikia nyimbo zao waishao kupigana. Hao wakusifu wewe kwa zaburi na kwa shangwe. Hata mimi nijalie nipate kufika kule.
4. Upungufu wangu wote ufunike wewe Bwana: niwe mtakatifu wako duniani hapa chini, nisikose kuingia furahani kwa wageni, uliowaita kuimba nyimbo za shangwe.
Comments
Post a Comment