211. Muumbaji wa Vitu Vyote



1. Muumbaji wa vitu vyote Baba, Mwana, na Roho, uletaye kila  siku, jua, mwezi, na nyota, ulindaye vizuri viumbe vyako vyote.


2. Ninakushukuru Baba, kwamba umenilinda, ukanikingia tena shida, woga, huzuni, hata hila ya mwovu haikunipoteza.


3. Niongoze Bwana wangu, kwa nenolo siku hii. Uwe mlinzi wangu leo, nisikose kukutii. Usiponiongoza sina budi kukosa.


4. Umtume malaika wako anishike vizuri, akazizuie hila, majaribu na tama. Naye anichukue mwisho kwako mbinguni.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu