209. Jua Likicha Linanyang’aza
1. Jua likicha linanyang’aza mashamba yetu kwa utukufu wa nuru yake yenye neema kuu. Nimelegea maungo usiku; sas ni macho, naona furaha nikitazama viumbe vyote.
2. Njooni tuimbe tukamtole Muumba sadaka za mioyo yetu, mambo mazuri tuliyonayo. Mungu ataka mioyo ya watu, nyimbo za sifa na za kumshukuru, ndizo sadaka zimpendaezazo.
3. Kazi ya Mungu ni kila siku kutubariki, kutuongoza, kutukingia hatari nyingi, sisi twalala, Bwana anakesha: tukiondoka, anatuangazia mwanga mzuri wa huruma yake.
4. Mambo ya watu w\yote yatapita. Mambo ya mingu yanasimama. Neno la Bwana lakaa milele. Atutolea wokovu wa neema, ayaondoa machungu ya kufa, tuwe wazima hapa na huko.
5. Mwenye huruma unisamehe makosa yangu, uyaondoe machoni pako kwa neema yako. Tena naomba: Nilinde vizuri, uniongoze na kunitawala kama mwenyewe unavyopenda.
6. Msiba na Shida mwisho zapita: kama twaona mwanga wa jua baada ya mvua mbinguni tena. Raha, uzima, furaha, amani zaningojea mbinguni kwa Mungu: Ninatamani furaha za juu.
Comments
Post a Comment