208. Ee Moyo Wangu Amka
1. Ee moyo wangu Amka, mwimbieni mwumba wako, aliyetupa neema, atulinde sote.
2. Nilipolala leo usiku, wewe Baba umenilinda vema, sikuwa na hatari.
3. Wasema: “Mtoto wangu, usiogope kitu, ulale usingizi, nitakuamsha kesho”.
4. Nimevipata vile ulivyoniambia. Naona mchana tena na nguvu na uzima.
5. Nilipe jinsi gani ulivyonitendea? Nakupa moyo wangu sina kizuri zaidi.
6. Huwezi kukataa kipaji kama hicho. Wajua kama sina mengine yakukupa.
7. Maliza kazi yako ulioanza kwangu, tuma malaika wako anikinge msiba.
8. Kubali nitendayo, unipe shauri jema, kuanza na kuisha ni shauri lako, Bwana.
9. Unibariki leo, nishike njia yako Nenolo la uzima liniongoze kwako.
Comments
Post a Comment