207. Lala Rafiki, Lala Mpenzi


1. Lala Rafiki, Lala Mpenzi laza kichwa chako kwa mwokozi. Lala vyema, lala usibgizi, Lala vyema.


2. Aa! Mpenzi sis twakupenda , si kama akupendavyo Bwana. Mapenzi yake yazidi sana. Lala, lala vyema.


3. Ulivyolala ni kama huamki kwa taabu tena. Raha kule utulivu sana. Lala, lala vyema.


4. Hata jua tukufu litoke hata watu wema wafufuke. Waje na Yesu waume, wake. Lala, lala vyema.


5. Siko kuagana, si ‘kwa heri’. Punde atakuja tumkiri. Uwe mmoja kwake wa heri. Lala, lala vyema.


6. Mpaka tuone mbele zake, na mavazi awapayo wake, Hata ya siri yafunuliwe. Lala, lala vyema.


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu