204. Wenye Mizigo Njooni
1. Wenye Mizigo njooni, nitawapumzisha. Tusikilize sauti sauti, sauti yake Bwana. Inatupa habari ya Baraka nyingi dhambi huondolewa, furaha inakaa.
2. Enyi wanyonge njooni nitawapa nguvu. Wote sikilizeni mbali na karibu Adui zetu wengi watupinga sana, kwa nguvu ya mwokozi wote watashinda.
3. Kila ajaye kwangu, simfukuzi kamwe. Sauti ya pendo hili yatufurahisha. Yesu aita wote walio na dhambi, wamjie wakapate raha ya mapenzi.
Comments
Post a Comment