203. Yesu Bwanangu Shujaa
1. Yesu Bwanangu Shujaa na mwokozi anaishi. Nikijua haya tu, ninaweza kutuliza moyo wangu ukiwa wenye woga wa kufa.
2. Yesu mwokozi wangu, Anaishi hata mimi nitaishi mahali, atakapokaa Bwanaangu, kwani viungo hukaa palipo kichwa chao.
3. Nimeungana naye, nikitumaini yeye. Ninamshika kwa nguvu, nikimtegemea kweli. Hata nguvu ya mauti hainitengi naye.
4. Mwili wangu wa sasa utaoza kuwa vumbi. Baadae na yeye atanifufua tena, niwe mbinguni kwake na kumuona milele.
5. Wenye unyonge hapa, kule watapata nguvu. Napandwa kwa aibu, kule nina utukufu. Ninapandwa kwa mwili, nitaishi kwa roho.
6. Furahini viungo vya mwokozi hampotei iacheni huzuni, ikilia panda kuu iwaamshapo wafu.
Comments
Post a Comment