202. Watu wote Yawapasa


1. Watu wote Yawapasa kufa kama Majani. Wakaao Duniani, yawapasa kuzikwa, na kuoza kaburini, na kuona furaha tulioahidiwa.


2. Hata mimi ni Tayari, nitamwekea Mungu roho yangu akitaka, kuniita kufani.  Kwani nimekombolewa na mwokozi wangu Yesu, kufa kwake kuchungu kumenipa tulizo.


3. Yesu amenikomboa akinifia mimi. Sasa mimi nitaacha kwa furaha duniani, na kuingia mbinguni kwake Mungu mwenye enzi, na kwa Yesu Mwokozi katika furaha kuu.


4. Kule wateule wengi wanapomtumikia Mungu penye kiti chake, ni mahali pazuri.  Na malaika waimbapo nyimbo za kumsifu Bwana: Ee mungu mtakatifu, Baba Mwana na roho.


5. Waliko wazee wa kale, wafumbuaji wa Mungu: kule wanakaa mitume juu ya viti vya enzi: kule wamekusanyika waliotangulia, kule tunasikia Haleluya daima.


6. Naona Yerusalemu unang’aa kwa Meanga mkuu Nasikia sauti nzuri za vinubi na nyimbo. Kweli ni furaha kubwa, kule jua litokapo unapopambazuka mchana usioisha.


7. Nimeona haya yote rohoni kwa furaha. Basi ninapenda kwenda kuingia mbinguni! Ndugu zangu: kwaherini! Mingu awalinde nyote. Kwaherini! Nakwenda, imekwisha safari.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu