201. Mwenzetu Kazi Yako Imekwisha
1. Mwenzetu kazi yako imekwisha duniani. Umekwisha kutua mzigo wa shida na taabu. Yesu tupe kufika walipo washindaji.
2. Yesu ni kiongozi katika bonde la kufa. Amekutangulia kaburini na peponi. Yesu tupe.
3. Wewe wachukuliwa na malaika kwa Mwokozi. Utapokelewa sasa na wateule wa Mungu. Yesu tupe…….
4. Mwili wako wazikwa, ugeuke kuwa vumbi. Twatumaini kwamba ufufuko utakuwa. Yesu tupe…………
5. Sasa unapandwa tu kama mbegu ya shambani. Mpaka yaje mavuno siku ya kufufuliwa. Yesu tupe…………….
Comments
Post a Comment