200. Sijui Saa ya Kufa Kwangu



1. Sijui Saa ya Kufa Kwangu, maisha yangu yapita. Naomba Mungu, Bwana wangu kwa ajili ya mwanao. Shika roho yangu, kwa furaha, niache ulimwengu huu.


2. Tukiwa hapa duniani kufa kunatuvizia, hakutuwekei kiaga, kunakuja kwa haraka. Shika roho……………


3. Unifundishe nifikiri, vizuri mambo yakufa. Nijutie makosa yangu, yaondolewe na Yesu. Shika roho…………….


4. Unipe nguvu, nijivike tayari kwa mambo yote. Niweze kuitika vema, ukiniita kwa kufa. Shika roho……….


5. Baba, ondoa dhambi zangu kwa damu ya Bwana Yesu. Najificha katika huyu, kwani amenikomboa. Shika roho……


6. Nikiwa naye Bwana Yesu sioni hofu ya kufa. Na saa ya kufa ikifika, namtumaini Yesu tu. Ninajua kwa damu ya Yesu Napata kufa kuzuri.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu