199. Nikifa Nitapata Uzima kwa Yesu

 


1. Nikifa nitapata uzima kwa Yesu. Ninampa moyo wangu, nife kwa furaha.


2. Napenda kwenda pale alipo Bwanangu, nikae mjini kwake siku za milele.


3. Nimeushinda sasa uchungu na woga, kwa damu ya Mwokozi nimekombolewa.


4. Zikipunguka nguvu, puzi ikiisha, nisaidie Bwana, nilale kwa raha.


5. Saa yangu ikifika, niiache dunia, unitulize Bwana, nichukue kwako.


6. Nikifika mbinguni, nitakuimbia na kukusifu Bwana, kwa furaha kubwa.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu