196. Upendo wa Mungu Wetu


1. Upendo wa Mungu wetu ndio jua letu. Hutung’azia moyoni hufuta uchungu, giza hukoma na mchana hutokea sasa, furaha tupu na shangwe huwamo moyoni. Upendo huu una nguvu tangu mwanzo na daima, atupenda mimi nawe, tuwe karibu nay eye.


2. Tangu mwanzo Baba Mungu alivyotuumba, ametuonyesha pendo kwa kutukumbuka. Hutupa mema mengi mno duniani petu, ila sisi hatukumpa shukrani ya kweli. Upendo huu…………….


3. Ndipo akamtuma Yesu mwenye pendo jingi. Awaza, “pendo la kufa, watalikubali”? atuamsha atuita, “acheni mabaya”! tumjue anavyopenda kutupa uzima. Upendo huu……………


4. Nasi tudumu pendoni Yesu Bwana wetu yeye jua la Baraka Baraka mioyoni mwetu. Tumwamini na tumpende sasa na milele. Amani tupu, rehema zatoka kwa Yesu. Upendo huu………..


Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu