192. Nyumba Hubarikiwa
1. Nyumba hubarikiwa ukaamo, Yesu, uliye mpenzi wa mioyo, wakukaribishapo kwa furaha, uliye mgeni wa heshima kuu. Mioyo yetu inapokupenda na macho yote yakungojapo, midomo yote ikuulizapo, na watu wote wanapokutii.
2. Nyumba hubarikiwa, mume na mke wanapopatana kukupenda wakikumbuka, kama wamepewa wokovu mmoja nawe, ee Yesu. Wakushikapo na kutegemea, wakati wa furaha na shida, wasipoacha njia ya uzima hata huzuni ikiwashika.
3. Nyumba hubarikiwa, wawekwamo watoto wakujue, wakutii. Uwapendaye na kuwabariki watoto walio kondoo wako. Wanapokusanyika wa nyumbani, wasikilize neno lako tu, wanaposhirikiana kuomba na kukufurahisha, mwokozi.
4. Nyumba hubarikiwa, wewe Bwana, ukiwa mwenzao furahani, namo shidani kwani unajua kuponya na kutuliza mioyo. Mpaka wamalizapo kazi yako na kuiacha dunia mwisho, wafike pale, mwenyewe ulipo katika nyumba ya Baba yako.
Comments
Post a Comment