189. Uuchunguze Ndani Yangu
1. Uuchunguze ndani yangu, iwe safi nia, kwangu kama kwako Mungu, idhihiri pia.
2. Uchunguze moyo wnagu unifunulie, yaliyomo ndani yangu, name niyajue.
3. Kwanza washa zako tambi, kumefunga giza, nijue ambavyo dhambi ni ya kuchukiza.
4. Uchunguze na mawazo, ni mbegu za mambo asili ya machukizo, maumbuo umbo.
5. Uzidi kuyachunguza katikati yangu. Hata uishe nifundisha udhaifu wangu.
6. Hapo nikikuinamia mbele zako Mungu, hakika nitakujua ndiwe mpenzi wangu.
Comments
Post a Comment