187. Kama Ulivyoagiza



1. Kama ulivyoagiza kabla kuuawa, hivi nitafanya, Bwana nitakukumbuka.


2. Wewe kwa ajili yangu ulitoa mwili katika mkate wako huu, nitaukumbuka.


3. Vivyo damu ya thamani wewe ulitoa. Katika kikombe hiki, nitaikumbuka.


4. Nitazamapo golgota, kuona msalaba, na kipaji cha kafara nitakikumbuka.


5. Siwezi kusahau jinsi ulivyoumia, kweli nikiwapo mzima nitakukumbuka.


6. Kwa hiyo nakungojea ee Bwana kwa kuwa ujapo mara ya pili utanikumbuka.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu