186. Mfalme wa Upendo Ndiye



1. Mfalme wa upendo ndiye anichungaye mimi, yeye ni wangu milele, ananipenda daima.


2. Kwenye maji ya uzima hunipeleka mimi katika malisho mema, anilisha siku zote.


3. Mara nyingi napotea kwa ukaidi wangu, naye ananitafuta, na kunirudisha kwake.


4. Kivuli cha kufa kwangu sitaogopa tena, ukiwa kwangu daima mashaka wayaondoa.


5. Wanitandika meza, naula mkate wako, nanywa katika kikombe nikumbuke kufa kwako.


6. Siku zangu zote hapa wema wako u vivyo. Nikubali mchunga mwema, nikuimbie milele.

Comments

Popular posts from this blog

72. Tumesikia Mbiu

51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu