184. Moyo Wangu Ujipambe
1. Moyo wangu ujipambe, acha mambo ya gizani. Kaza mwendo wa nuruni hivi utang’aa vizuri. Kwani Bwana wa rehema akukaribisha kwake. Mwenye utukufu mwingi anapenda kuja kwako.
2. Amka ukamlaki yeye, umkaribishe vizuri. Abishaye hodi kwako, akuleteaye neema. Umkubali kwa furaha aingiaye moyoni. Sema: Bwana, nakupenda, sikuachi siku zote.
3. Hatuwezi kufahamu mambo haya ya ajabu; unapenda kuwa nasi kwa mkate na kwa mvinyo. Yesu tunaomba sana: wewe kaa leo hapa, tugawie neema yako, chakula kitakatifu.
4. Yesu, jua la rehema, Yesu chemchem ya uzima, Yesu, nakupenda sana, nuru ya maisha yangu. Nakuomba; nibariki nikila chakula chako nipe nguvu ya uzima, tuishi wewe na mimi.
5. Pendo limekuhimiza kutafuta wakosaji. Umetoa mwili wako kutulisha roho zetu, ukamwaga damu pia ili utunyweshe sisi. Twakumbuka pendo hili hapa karamuni kwako.
6. Yesu, mkate wa uzima, nijalie nisikose msaada wa karama yako, nisijiponze nikila. Nikumbuke, mabo haya yaonyesha pendo lako. Unisaidie, niwe mgeni wako kwa milele.
Comments
Post a Comment