183. Usiku Ulipotolewa
1. Usiku ulipotolewa, Yesu, umetugawia mapato ya mateso yako, tukumbuke kufa kwako. Waaminio wakusifu wakija karamuni kwako.
2. Tunakumbuka kufa kwako, tukila mwili wako huu; twapewa nguvu yako hii. Karamu hii tunayopewa yatuonyesha pendo lako.
3. Huu mkate ni chakula kweli, hii damu yatutuliza; mioyo yetu yapumzishwa tukila mezani kwako. Tunaongezwa nguvu zetu, za kukutegemea vema.
4. Twashirikiana na wote walio viungo vyako; kwani tunashibishwa sote kw amwili na damu moja, tu kundila Mchungaji mmoja; kwa hivi twapatana sote.
5. Twapewa mwili wako Bwana, tujue kweli ya kwamba miili yetu ya unyonge itageuka vizuri. Tutapokea mwisho kwako miili mipya ya uzima.
6. Watupa mema mengi Bwana Mwana Kondoo wake Mungu, mwenyewe u chakula chetu, kweli twatunzwa vizuri. Twakila hapa kwa uchungu, lakini kwako kwa furaha.
Comments
Post a Comment