179. Yesu Kwa Imani
1. Yesu kwa imani, nakutumaini, peke yako. Nisikie sasa na kunitakasa, ni wako kabisa tangu leo.
2. Nipe nguvu pia za kusaidia moyo wangu. Ulikufa wewe, wokovu nipewe, nakupenda wewe, Bwana wangu.
3. Hapa nazunguka katika mashaka, na matata. Palipo na giza utaniongoza hivi nitaweza kufuata.
4. Takuwa mzima nivushe salama mautini. Sina hofu kamwe ukiwapo name, name nikwandame siku zote.
Comments
Post a Comment