176. Tumiminie ee Mtakatifu
1. Tumiminie ee Mtakatifu, Roho wako mwenye nguvu atakase mioyo yetu, tuwe wako tu kale na kale!
2. Wewe mwenyewe, tulinganishe tuungame kwa furaha, ya kuwa u Bwana wetu, tena Mwokozi kwa damu yako!
3. Tukutazame kwa mioyo yote, tukilirudisha upya agano la ubatizo, tukufuate, tuache yetu!
4. Tukija sasa kubarikiwa, sikia kuomba kwetu, tugawie mema mengi, tutengemane mwangani mwako!
5. Na atujie Roho wa Bwana, atuunganishe sote kuwa kundi takatifu mpaka tumwone kwake mbinguni!
Comments
Post a Comment