175. Heri Kumjua Yesu, Bwana
1. Heri kumjua Yesu, Bwana.
Roho huamka, aniita.
Anitambua mali yake,
hanipotezi, niko kwake.
Msimuliwe sifa zake;
hana mwenzake, mponya pekee,
afurahisha moyo kweli.
Yeye ni yesu, tumtukuze.
2. Nikimwambia mambo yote
anituliza moyo vema
nikimfanyia kazi zangu,
anibariki hapa na juu. Msimuliwe…………..
3. Nikimjutia nimekosa,
anaondoa na mashaka.
Yeye hapendi nikishindwa,
anipa nguvu za kwendea. Msimuliwe
Comments
Post a Comment